
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Mshambuliaji wa mabingwa wa Ligi Kuu Bara Yanga Saimon Msuva ambaye kwa
sasa ameibua minong'ono mingi kwa mashabiki kuwa anaipenda timu ya Simba
kuliko ile ya Yanga anayochezea, amenyoosha maelezo kuhusu tuhuma hizo.
Akijibu maswali ya mashabiki kupitia kipengele cha KIKAANGONI cha
EATV, Msuva amesema yeye siyo shabiki wa Simba kama wengi wanavyodhani,
isipokuwa amelelewa kwenye familia yenye ushabiki na mapenzi kwa Simba.
"Mi sio shabiki wa Simba kwanza mjue hilo, lakini nimekulia kwenye
mazingira ambayo baba yangu mwenyewe kwanza ni shabiki mkubwa wa Simba,
nachezea Yanga na nina mkataba na Yanga, hivyo niko Yanga, hayo mengine
hayana ukweli wowote", alisema Msuva.
Msuva aliendelea kwa kusema kuwa yeye kama mchezaji anatamani
kuichezea timu hiyo kwani Simba ni timu kubwa kama ilivyo Yanga na Azam,
hivyo haina ubaya wowote kwa yeye kutamani kuchezea Simba.
"Siyo kwamba sitamani kucheza Simba, Simba ni timu kama Yanga au
Azam, ni timu kubwa zaidi na timu nzuri pia, naitamani Simba lakini kwa
sasa watu watambue nina mkataba na Yanga na naichezea Yanga".
Aidha Msuva amewakaribisha viongozi wa Simba kufanya mazungumzo na
Yanga kama watamuhitaji, na yeye yuko tayari kuhamia Simba endapo timu
hizo zitakubaliana huku akiweka wazi kuwa aliyekuwa mshambuliaji wa
Simba Mussa Hassan 'Mgosi' ndiye aliyemvutia yeye kuingia katika soka.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: