KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amesema timu yake haijashuka kiwango kama ambavyo baadhi ya wadau wa soka wanavyodai na kuongeza kuwa muda si mrefu watarudi katika ubora wao.


Baadhi ya wadau na wachambuzi wa soka kwa siku za karibuni wamekuwa wakitoa maoni yao kuwa Yanga imekwisha na wengine wakidai imechoka kutokana na wachezaji wengi kutopata muda wa kupumzika baada ya kutoka kwenye mashindano ya kimataifa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alisema muda sio mrefu watarudi tena na itadhihirika kama kweli wamechoka ama la.

β€œSio kweli kama tumekwisha, tuko vizuri na muda sio mrefu mtaona mambo mazuri, tunaendelea kujipanga na kurekebisha mapungufu yetu kuhakikisha tunafanya vizuri,”alisema.

Yanga imetoka kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Matokeo hayo yameishusha kutoka nafasi ya tatu hadi ya tano ikiwa na pointi 11 sawa na Azam FC ambao wanashika nafasi ya sita, lakini Yanga ikiwa nyuma mchezo mmoja.

Timu zinazoongoza nne bora ni Simba yenye pointi 17, Stand United 15, Mtibwa Sugar 13 na Kagera Sugar yenye pointi 12.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: