Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Sh Trilioni 1.37 mwezi Septemba mwaka huu na kufanya fedha zilizokusanywa katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka mpya wa fedha wa 2016/2017 kufikia sh trilioni 3.59.


Kayombo alisema kwa mwaka huu wa fedha TRA imeweka malengo ya kukusanya kodi sh Trilioni 15.1 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali ili kufanikisha malengo ya serikali katika kuhudumia wananchi.

“Mwezi Agosti tulifanikiwa kukusanya kiasi cha Sh Trilioni 1.13 hivyo mtaweza kuona ni namna gani tumevuka makusanyo ya miezi miwili iliyopita ya Julai na Agosti kwa kufikisha Sh trilioni 1.37,”alisema Kayombo.

Alisema ukusanyaji wa mapato ya serikali unaenda sambamba na kuelimisha wananchi kuhusu wajibu wao wa kulipa kodi sahihi na kwa wakati hivyo.

Wasafirishaji wa mizigo kwenda mikoani wanahimizwa kudai risiti za EFDs pindi wanaponunua bidhaa na kuwa nazo wakati wanasafirisha mizigo ili kuepuka usumbufu pale wanapohitajika kuonyesha risiti hizo.

 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: