Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, imemhukumu mtoto wa Mbunge wa Mbarali, Haroon Mulla Pirmohamed (CCM) kulipa faini ya Sh138,390,000 au kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kukiri kosa na kutiwa hatiani kwa kumiliki nyara mbalimbali za Serikali.


Katika kesi hiyo, mtoto huyo Pirmohamed Haroon alikutwa akimiliki kilo 46 za nyama ya tandala, mbawala, swala pala, tohe, njiwa pori, kanga pori na pembe za tandala na tohe vyote vikiwa na thamani ya Sh138,390,000.

Akisoma hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alimhukumu mshtakiwa huyo kulipa faini hiyo ambayo ni mara 10 ya thamani ya nyara alizokutwa nazo na iwapo atashindwa atumikie kifungo cha miaka 20.

Hata hivyo, baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Haroon alikwepa adhabu ya kifungo kwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kupatiwa risiti ya malipo ya Serikali namba 8870022.


DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: