
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Siku tatu baada ya Katibu wa Kamati ya Muafaka ya Wazee wa Yanga,
Ibrahim Akilimali kusema kuwa Yanga haiwezi kukodishwa kama masufuria ya
kwenda shughulini, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji amezungumza kuhusu
mkutano mkuu wa Yanga na kugusia kuhusu ushiriki wa Mzee Akilimali kama
atashiriki au hatashiriki.
Manji amesema kuwa kuna taarifa ameiona sehemu ikielezea kuwa Mzee
Akilimali hajalipa ada ya uanachama wa Yanga na hilo kama lina ukweli
basi kwa mujibu wa katiba ya Yanga hataruhusiwa kushiriki mkutano huo
ambao utafanyika Jumapili.
“Nimeona habari sehemu imesema kuwa hajalipa ada ya uanachama kwa
miezi sita, sina hakika ila kama ni kweli hataruhusiwa kushiriki kwenye
mkutano, na hilo sijalipanga mimi ni katiba ya Yanga ndiyo inasema
hivyo, mimi sina mamlaka ya kupindisha katiba,” amesema Manji.
Aidha Manji amezungumza kuhusu mkutano mkuu na kuwataka wanachama wa
Yanga kujitokeza kwa wingi ili waweze kufanya maamuzi ya pamoja ambayo
yatakuwa na faida kwa klabu na kwa ambao bado hawajasoma taarifa ya
makubaliano ya Yanga na kampuni ya Yanga Yetu basi watapatiwa taarifa
hizo wazisome kabla ya mkutano.
“Kama mwanachama hajalipa kadi kwa kipindi cha miezi sita afike kwa
viongozi wa matawi kuomba tena nafasi ili ikiwezekana na yeye ahudhurie
mkutano, wanachama waje tujue ni maamuzi gani tutafanya, ulinzi upo wa
kutosha na ambao bado hawajasoma taarifa wanaweza kufika ofisi za klabu
saa 7:30 asubuhi tutakuwa tumeshafungua ofisi,” alisema Manji.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: