HASHIM Rungwe, Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), amesema chama hicho kipo mbioni kujiunga na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wowote kuanzia sasa.


Rungwe ambaye pia alikuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHAUMMA katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, amesema kuwa hakuna mtu yoyote timamu anayeweza kubeza mafanikio ya muungano wa vyama vya UKAWA.

“UKAWA imeleta mafanikio makubwa sana kwa vyama vya upinzani, hakuna mtu aliye timamu anaweza kubeza hilo. Sisi kama CHAUMMA, tupo kwenye mchakato wa kuangalia namna ya kuunganisha nguvu na UKAWA,” amesema Rungwe.

Rungwe alikuwa akizungumza asubuhi ya leo katika kipindi cha Power Breakfast, ambacho hurushwa na kituo cha Clouds Fm. Pamoja na mambo mengine pia ameelezea namna alivyokuwa akimuombea kura mgombea Urais wa CHADEMA, aliyekuwa akiungwa mkono na vyama vya UKAWA katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

“Licha ya mimi kugombea urais, lakini kila nilipopita katika mikutano yangu nilikuwa nikiwambia wananchi, kama wanaona mimi sifai kuwa rais wa nchi basi wamchague mgombea wa UKAWA, mimi nilikuwa nikipambana na Chama Cha Mapinduzi tu,” amesema.

Alipoulizwa, kwanini chama chake kiliamua kusimamisha mgombea ilihali kilikuwa na imani na mgombea urais wa UKAWA, Rungwe amesema CHAUMMA kilikuwa chama kipya kilichohitaji kujitambulisha kwa watanzania.

“Chama cha siasa hakiendeshwi kwa one man show (uamuzi wa mtu mmoja), bali kwa maamuzi ya vikao vya chama, kwa kuwa sisi tulikuwa bado chama kipya cha siasa tuliamua tusimamishe mgombea urais na kwakweli tumefanikiwa kujitambulisha,” amesema.


DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: