Klabu ya Simba SC imethibitisha kuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo unafanyika leo.


Mkutano huo mkuu maalum wa klabu utakuwa na lengo moja tu ambalo ni kumtangaza mzabuni aliyeshinda kumliki sehemu ya klabu kupitia mfumo wa hisa ambao utaanza kutumika kuendesha klabu hiyo.

Taarifa iliyotolewa jana na klabu hiyo imeeleza kuwa, β€œKwenye mkutano huu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi”.

Simba tayari imeshapitia hatua mbalimbali za ubadilishaji wa uendeshaji na umiliki wa klabu ambapo serikali na shirikisho la soka nchini TFF vimebariki mabadiliko hayo kwa manufaa ya maendeleo ya soka nchini.

Mkutano huo maalum utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam na historia itaandikwa kwa mara ya kwanza katika soka la Tanzania.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: