WAKATI Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, akidaiwa kupewa mechi mbili kukinusuru kibarua chake, mshambuliaji hatari wa timu hiyo, Emmanuel Okwi, amesema kuwa, iwapo atakuwa akipangwa pamoja na John Bocco, hakuna shaka kuwa mwalimu wao huyo hatang’oka Msimbazi.


Akizungumza na BINGWA jana, Okwi alisema kuwa, japo Simba ina washambuliaji wengi wazuri na wenye uwezo wa kuibeba timu hiyo, lakini anapocheza na Bocco katika safu ya ushambuliaji, kombinesheni yao inanoga zaidi.

Kikosi cha Simba kimewasili  jijini Mbeya kwa ajili ya mechi ya dhidi ya Mbeya City, ambapo imedaiwa Omog ametakiwa kuhakikisha anashinda mchezo huo pamoja na ule unaofuata dhidi ya Prisons ya huko, zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine.

Akizungumzia mechi hiyo na hali inayomkabili Omog, Okwi alisema: “Hatuna sababu ya kushindwa kupata pointi sita Mbeya, kikosi chetu kipo vizuri, kikiwa na wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu kuanzia ulinzi, kiungo na safu ya ushambuliaji.”

Alipoulizwa alivyojipanga kuibeba Simba katika mechi zao zote zijazo jijini Mbeya, alisema: “Binafsi sina uwezo wa kuisaidia timu, mimi kama mimi, ninategemea ushirikiano wa wenzangu, ila kama nikipangwa pamoja na Bocco, mambo lazima yawe mazuri.”

Kwa upande wake, Omog alisema kikosi chake kipo vizuri na amefanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika michezo ya awali na kuhakikisha anapata pointi tatu katika mchezo na Mbeya City kesho na hata ujao dhidi ya Prisons.

Alisema hakuna mechi rahisi kwao, lakini pia anajivunia uelewano mzuri baini ya wachezaji wake, hasa katika safu ya ushambuliaji.

“Vijana wangu wapo vizuri na tunakwenda kutafuta pointi tatu muhimu katika mchezo wetu dhidi ya Mbeya City, baada ya mapumziko mafupi tutakutana na Tanzania Prisons, ambako nako ni muhimu kupata pointi,” alisema.

Alisema msimu uliopita walirejea Dar es Salaam na pointi tatu kutoka Mbeya City, baada ya kupoteza tatu kwa Prisons, jambo ambalo kwa sasa hawataki lijirudie, hasa kwa wakati huu wakiwa katika vita kubwa ya kupigania kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara.

Simba wapo kileleni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mabao, baada ya kulingana pointi na timu nne ambazo ni Yanga, Mtibwa Sugar na Azam, zote zikiwa na pointi 16, baada ya kushuka dimbani mara nane.


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: