WACHEZAJI wawili muhimu ndani ya kikosi cha Simba, Emmanuel Okwi na Jjuuko Murushid, ambao waliukosa mchezo uliopita dhidi ya Prisons, kutokana na kuwa nchini kwao Uganda, sasa wamerejea na wapo tayari kwa mapambano.


Wawili hao walikuwa kwenye kikosi cha timu yao ya Taifa ya Uganda, ‘The Crane,’ huku Okwi akidai kuwa na majeraha, lakini sasa wamewasili tayari kuwawinda Lipuli FC, mchezo unaotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii kwenye Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti la  DIMBA Jumatano jana, Meneja wa timu hiyo, Richard Robert, alithibitisha kuwa, wachezaji hao wapo nchini na kwamba wapo tayari kwa mapambano, hasa mchezo dhidi ya Lipuli.

“Tunashukuru kwamba wachezaji wetu hao wameshawasili na wapo tayari kwa mapambano, Okwi alikuwa majeruhi, lakini imeonekana hayakuwa makubwa, lakini Jjuuko yeye yupo fiti kabisa,” alisema.

Richard alisema kikosi cha timu yao kipo vizuri na wanachokisubiri ni siku hiyo ya kuwakabili Lipuli, kwani malengo yao ni kuhakikisha kila mchezo wanaibuka na ushindi mpaka watakapotwaa ubingwa.

Simba wataingia katika mchezo huo wakiwa na ari baada ya kutoka kuzifunga timu za Mbeya, yaani Mbeya City waliowafunga bao 1-0, wakapata tena ushindi kama huo dhidi ya Tanzania Prisons.


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: