NAHODHA wa Prisons, Laurian Mpalile, amefichua siri ya kufungwa bao 1-0 na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wiki iliyopita.


Akizungumza na gazeti la BINGWA , Mpalile alisema alijua mshambuliaji wa Simba, John Bocco, angewafunga katika mchezo huo.

Mpalile alisema Bocco hakubahatisha kuwafunga, kwani  amekuwa  akiwafunga mara nyingi kila  wanapokutana.

Alisema Bocco ni mchezaji anayewasumbua kwa muda mrefu tangu akiwa anaitumikia Azam FC alikuwa anawafunga nyumbani na ugenini.

Mpalile alisema wamekuwa wakijitahidi kumdhibiti mshambuliaji huyo, lakini ni mara chache wanafanikiwa kumzuia.

Alisema walijua mapema Bocco angewafunga na ndicho kilichotokea katika mchezo wao wa Jumamosi iliyopita.

β€œSijui tuseme Bocco ana bahati ya kutufunga au vipi kwa sababu kila tunapokutana naye kwenye mechi lazima atufunge, ametufunga zaidi ya mara tatu, Chamazi na Sokoine,” alisema Mpalile.

Alisema katika mchezo wa marudiano itabidi wajipange ili makosa yasirudie na baadaye kuondoka na ushindi.

Simba kwa sasa wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 22 sawa na Azam, lakini wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: