Mshambuliaji wa Simba, Mghana Nicholas Gyan alisajiliwa akitokea katika klabu ya Ebusua Dwarfs ya Ghana amesema mashabiki wa Simba wasiwe na hofu mambo mazuri yanakuja kutoka kwake.

Gyan tangu kutua hapa nchini ameshindwa kufanya kile ambacho mashabiki wengi wa Simba walikuwa wakitegemea makubwa kutoka kwake kwa umahiri wake wa kutupia nyavuni.

Katika mazoezi ya Simba ambayo yanaendelea katika uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini, Gyan anaonekana kuimarika.

Kocha wa Simba, Joseph Omog na msaidizi wake Masoud Djuma walikuwa wakifurahishwa na kiwango ambacho alionyesha Gyan katika mazoezi hayo na muda mwingine walikuwa wakimpigia makofi kwa kuwa alikuwa akifanya vizuri.

“Nimemaliza matatizo yaliyokuwa nyumbani na hata ambayo nilikutana nayo hapa nchini. Kitu kingine ambacho kimechangia kuwa kama hivi ni viwanja vya hapa eneo la kuchezea ni gumu kuliko ambavyo nimezoea kucheza kule kwetu,” alisema Mghana.

“Simba ni timu kubwa yenye presha ya mashabiki, kuliko timu ambayo nilikuwa nikicheza hapo awali, lakini kila kitu nimeshakizoea sasa na kilichobaki mimi kuanza kazi ile ambayo imenileta hapa nchini,” alisema Gyan.

“Nimezungumza naye tukiwa wawili tu, kabla ya wiki hii na alinihakikishia kila kitu kipo sawa na jukumu limebaki kwake kuanza kufanya kazi ambayo benchi la ufundi na mashabiki wa Simba wanahitaji kutoka kwake,” alisema Omog.

Djuma alisema kama mchezaji anaashindwa kufanya vizuri na kabla ya hapo alikuwa akifanya vizuri ujue anashida ambayo inamsumbua na hata kwa Gyan alikuwa hivyo kwani kila mara kabla ya mazoezi nilikuwa nikizungumza nae.

“Licha ya matatizo ambayo aliokuwa nayo, alikuwa anaimani nyingine ambazo zilimtoa katika hali ya kimchezo lakini nimemshauri aachane na hivyo vitu afanye kazi ambayo imemleta Simba na wiki yote hii katika wachezaji waliofanya vizuri mazoezini yeye ni mmoja wapo,” alisema Djuma.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: