SHEIKH Issa Ponda amepewa siku tatu na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, awe amejisalimisha kwa chombo hicho cha dola kwa madai ya kufanya uchochezi juzi.


Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Sheikh Ponda ambaye pia ni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, anadaiwa kutoa kauli za kichochezi na zisizofaa katika jamii.

Kamanda Mambosasa alisema jijini jana kuwa kitendo cha Sheikh Ponda kulikimbia Jeshi la Polisi baada ya mkutano huo hakitamsaidia na kwamba ni heri ajisalimishe, "ili awe sehemu salama".

Alisema jeshi hilo halikufanikiwa kumnasa wakati wa mkutano wake huo na waandishi wa habari kwa kuwa halikupata taarifa sahihi kuhusu mkutano huo na muda wa kufanyika kwake.

"(Waandishi) wengine mliambiwa mkutano huu ungefanyika saa nne asubuhi, lakini ulianza mapema hivyo tulimkosa kidogo tu kumkamata," alisema Mambosasa. "Akijisalimisha kabla ya siku hizi tatu itakuwa ni salama zaidi."

Katika mkutano wake wa juzi uliofanyika Kariakoo jijini, Sheikh Ponda alieleza ziara yake ya jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa

Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na mikakati ya mtaalamu huyo wa sheria kurejea katika siasa baada ya kupona.

Pia alizungumzia hali ya usalama na siasa nchini.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: