Mesut Ozil amewajibu wadau wanaoponda kiwango chake akidai amekuwa akicheza kwa nguvu zote na mepenzi makubwa Arsenal.
Kauli ya Mjerumani huyo imekuja, baada ya wadau kukosoa uchezaji wake wakidai hana msaada Emirates licha ya kununuliwa kwa bei mbaya kutoka Real Madrid kwa Pauni 42 milioni akiwa ndiye mchezaji ghali zaidi kununuliwa na klabu hiyo.
"Siku zote nimekuwa nikijitahidi kuifanyia mambo makubwa Arsenal, lakini sina furaha katika nafasi ya uwanjani ninayopangwa,"alisema Ozil mwenye miaka 29.
Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na mpango wa kumfuata bosi wake wa zamani Jose Mourinho kujiunga na Manchester United katika dirisha dogo Januari, mwakani.
Mkataba wake unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu huu na Arsenal imemuweka sokoni ikitaka kumpiga bei mapema ili kupata fedha.



Post A Comment: