Kocha wa Simba, Joseph Omog amesema anaifahamu vyema Mtibwa Sugar kuwa ni timu nzuri na ina wachezaji bora hivyo haitakuwa mechi rahisi kushinda, lakini lazima waondoke na ushindi leo.

Mechi hiyo inawakutanisha Simba na Mtibwa kwenye uwanja wa uhuru ikiwa ni siku moja baada ya mechi ya watani zao Yanga walioibuka na ushindi jana Jumamosi.

Matokeo ya Yanga ya mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar yanawapa presha Simba kucheza kufa na kupona ili kuibuka na pointi tatu zinazoweza kuwarejesha kileleni mwa msimano wa Ligi Kuu leo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: