ads

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi amesema tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba amenunuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hazina ukweli.


Katambi ambaye juzi alitangaza kujiunga na CCM ametoa kauli hiyo kipindi ambacho kumekuwa na tuhuma zinazoelekezwa kwake  ikiwamo ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwamba ameshawishiwa na akakubali.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi jana Novemba 22, Katambi amesema hakuna mtu yoyote anayeweza kumnunua huku akisema Chadema kimepoteza dira hivyo wenye uelewa wataondoka.

“Nimesikia mengi, nitafanya mkutano na waandishi wa habari, nilidhani wangejitathimini katika ukweli ili kusaidia vijana, chama na taifa lakini kama wanaamua kushambulia mtu kwa uongo bila ushahidi, nitasema ukweli waziwazi,” amesema Katambi

Kuhusu tuhuma za rushwa, Katambi amesema ‘’Katambi hanunuliki wala hana bei naishi katika Principle…kwa wenye akili wangejua dira imepotea watafute upya masafa.”

Awali jana asubuhi, Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni akizungumza  na Mwananchi kuhusu kuondoka kwa Katambi amesema;

"Badala ya nguvu na fedha kuzielekeza kujenga viwanda wao nguvu wamezielekeza kushawishi viongozi wetu, wamewashwishi wengi na Katambi ni miongoni ingawa wengine wamekataa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: