
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amemuomba Rais John Magufuli kutafakari upya kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, bado anafaa kuongoza Wizara hiyo, kufuatia wimbi la matukio yanayoashiria ukosefu wa usalama nchini.
Lema, ambaye ni waziri kivuli wa wizara hiyo, alisema hayo jana, wakati akizungumzia kauli za Mwigulu aliyoitoa juzi kuhusu kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na matukio mengine, yakiwamo ya kupotea kwa aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Ben Saanane.
“Jana (juzi) nilifikiria Mwigulu angeachana na ngonjera zake akaongelea habari angalau ya maslahi ya askari hawa, Mwigulu amenisikitisha sana, na sidhani kama anastahili kukaa kwenye ile ofisi hata kwa saa mbili.
“Yeye kama Waziri wa Mambo ya Ndani, tangu Lissu ameshambuliwa hajawahi kurusha hata mguu Nairobi, hata kwenda kuongea na Waziri wa Mambo ya Ndani Kenya, kuomba ulinzi kwa ajili ya mgonjwa.
“Wakati ni mbunge mwenzake, tena wa mkoa wake amepigwa risasi, ila hajishulishi, jana anaongea vitu vyepesi kuhusu maisha ya watu, kwa kauli zake kama
kuna mtu alimtazama wakati anaongea, utajua tukio la Lissu limefanywa na nani, na nani yuko nyuma ya tukio hili, vinginevyo angekuwa na ujasiri wa kuelekeza polisi kutafuta wahalifu kwa nguvu zote, angewaza pengeni anayefuata ni yeye,” aliongeza.
“Serikali ijue tu kama tukio hili la Lissu haliko connected na wao, waliofanya tukio hili wana nia mbaya,” alisema Lema.
Post A Comment: