Kocha wa Simba, Joseph Omog amewafanyisha mazoezi wachezaji wake katika mvua kubwa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


 Simba imeweka kambi visiwani humo kujiandaa na mchezo wake wa watani wa jadi Yanga utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Amaan wachezaji hao walilazimika kusubili kwa nusu saa kabla ya kuanza mazoezi kutokana na mvua hiyo.

Baada ya mvua kupungua kidogo benchi la ufundi la Simba chini ya kocha Omog walishauriani takribani dakika kumi kabla ya kutoa uamuzi wa kufanya mazoezi pamoja na hali hiyo.

Baada ya kikao hiko kifupi waliamua kufanya mazoezi mapesi mapesi kutokana na uwanja huo wa Amaan kujaa maji kwenye eneo la kuchezea.

Akizungumza baada ya mazoezi hayo kocha Omog alisema wachezaji kufanya mazoezi katika hali ya ubaridi kama iliyokuwa huku visiwani Zanzibar inaongeza morali kwa wachezaji kufanya mazoezi zaidi.

"Ukiondoa siku hizi mbili ambazo mvua imenyesha kwa mfulululizo tumefanya mazoezi mengi kutokana na hali ya hewa hii na wachezaji huwa wanajengeka zaidi," alisema Omog.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: