KITENDO cha winga wa Simba, Shiza Kichuya kuendelea kutamba hasa anapokutana na Yanga, kimeiweka Simba kwenye wakati mgumu kuzungumza naye kuhusu mkataba mpya.


Kichuya aliyejiunga na Simba mwaka jana akitokea Mtibwa Sugar kwa ada ya usajili ya kawaida, amekuwa moto klabuni hapo na kuiweka timu hiyo katika hali ngumu wakati huu akielekea mwishoni mwa mkataba wake. Kichuya alisaini Simba miaka miwili na huu ndiyo msimu wa mwisho klabuni hapo.

Simba ilifanya usajili mkubwa msimu huu kuwashusha nyota wa maana wakiwemo Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima waliogharimu zaidi ya Sh 150 milioni, lakini Kichuya ameendelea kuwa staa mkubwa zaidi klabuni hapo jambo ambalo linawafanya kuanza kujipanga kumpatia mkataba mnono.

Tangu amejiunga na Simba mwaka jana, Kichuya ameifungia timu hiyo mabao 16 Ligi Kuu na moja katika kombe la FA hivyo kuwa mchezaji aliyefunga zaidi klabuni hapo katika kipindi cha miezi 14 iliyopita.

Katibu Mkuu wa Simba, Dk.Anord Kashembe alisema; "Siwezi kusema kama anastahili mkataba mnono ama la, naamini Kamati ya Usajili imeona anachofanya na itafanya kazi yake."

"Kama klabu tumejipanga kuhakikisha hatuwapotezi wachezaji hao wanaoelekea mwishoni mwa mikataba yao. Sina nafasi kubwa sana ya kusema kwani hilo suala linafanywa na Kamati ya Usajili ambayo inajitegemea," alisema Katibu huyo msomi zaidi kwa klabu za Ligi Kuu Bara.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: