Mechi mbili za kuamua hatma ya washambuliaji Mrundi Laudit Mavugo na Mghana Nicholas Gyan katika kikosi cha Simba.


Mmoja kati ya washambuliaji hao wawili atafungasha virago kumpisha Mnigeria Mussalawal Ibrahim  kuingia katika kikosi cha Simba wakati wa kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili Novemba 15.

Simba kwa sasa inaendelea na maandalizi yake ya kujindaa na mechi yake dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine na wiki moja baadae watacheza tena na Tanzania Prison katika uwanja huo.

Simba baada ya kucheza mechi dhidi ya Prison dirisha dogo la usajili litafunguliwa na huenda kuna moja ya mchezaji wa kigeni kuachwa na kiingizwa jina la Mnigeria Ibrahim.

Ibrahim amejiunga na Simba na kufanya mazoezi nayo tangu akiwa Zanzibar kama kocha Joseph Omog atalizika na kiwango chake basi lazima kumuondoa mchezaji mmoja wa kigeni.

Bila shaka kati ya Mrundi Mavugo na Mghana Gyan mmoja wao ataachwa ili kumpisha Ibrahim.

Mkataba wa Mavugo unamalizika mwisho wa msimu huu na ameshindwa kabisa kufikia ubora wake wa msimu uliopita kwani hadi sasa ameshafunga mabao mawili tu.

Gyan alisajiliwa na Simba kwa mbwembwe akitokea nchini Ghana katika klabu Ebusua Dwarfs akiwa  mfungaji bora, lakini tangu alipotua nchini ameshindwa kabisa kuonyesha makali yake.

Bila shaka nafasi ya Ibrahim ipo wazi, lakini kama ataweza kumlizisha kocha  Omog na msaidizi wake Masoud Djuma katika mazoezi ambayo anaendelea kufanya na kikosi hiko tangu alipojiunga wakiwa Zanzibar.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: