Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataja askari wawili waliouawa na kundi la wapiganaji la ADF wakati wakilinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).


Askari hao wametajwa kuwa ni Koplo Maselino Paschal Fubusi na Praiveti Venance Moses Chimboni.

Imeelezwa askari wengine 12 wamejeruhiwa katika shambulio lililofanywa na kundi hilo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya JWTZ iliyotolewa jana Jumanne imesema, β€œAskari hao wamefariki baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi, tukio lililotokea Oktoba 9 umbali wa kilomita 24 mashariki mwa mji wa Beni.”

Amesema, β€œMajeshi yetu yamewarudisha nyuma waasi hao na kudhibiti eneo. Kutokana na shambulio hilo, Umoja wa Mataifa umeunda bodi ya uchunguzi wa tukio hilo,” imesema taarifa hiyo.

Imeelezwa maofisa na askari wa JWTZ wanaendelea kutekeleza majukumu yao katika operesheni hiyo.

Kuhusu miili ya askari hao kurejeshwa nchini, taarifa imesema Umoja wa Mataifa unaandaa utaratibu na itakapokamilisha wataujulisha umma mapokezi, kuaga na mazishi yatakavyokuwa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: