
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
HALMASHAURI ya Mji kibaha imeanza ujenzi wa stendi kubwa ya kisasa ya mabasi yaendayo mkoani, itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.4.
Ujenzi huo unafanyika kutokana na stendi ya awali kuwa katika eneo la hifadhi ya barabara Kuu ya Dar es Salaam-Morogoro.
Ujenzi huo uko katika hatua za awali na utakuwa wa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilka mwishoni mwa mwezi Desemba ama mwanzoni mwa Januari 2018.
Ofisa Habari wa Halmashauri hiyo, Innocent Byarugaba, alifafanua ujenzi wa stendi hiyo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa uendelezaji majiji na kuwa mkandarasi ni Kampuni ya MS Group Six ya Dar es Salaam.
Alisema stend hiyo ya kisasa itakuwa na uwezo wa kuingiza mabasi makubwa ya mikoani 60, mabasi ya kati 48, teksi 20, bajaji 10 na magari binafsi kwa ajili ya wanaopokea na kusindikiza wasafiri.
βTunatarajia pia stendi hii itakuwa na jengo la utawala, mgahawa, ofisi za kukatia tiketi, kituo cha mafuta na miundombinu kwa ajili ya wenzetu wenye mahitaji maalum, lakini pia gereji kwa ajili ya kutengeneza magari yatakayokuwa yanaharibika,β alisema Byarugaba.
Pia itakuwa na mashine za kutolea fedha ATM, mahali pa kupumzikia abiria na kwa awamu ya kwanza itakuwa na miundombinu iliyojitosheleza kuanza kutumika kwa maana ya uzio, kituo cha polisi, kizimba cha taka na miundombinu ya kukusanya ushuru .
Post A Comment: