Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba amesema hatakuwa na sababu ya kuendelea kuwa waziri endapo Watanzania watakosa ugali juu ya meza.


Dk Tizeba amesema hayo jana Alhamisi wakati wa mkutano wa saba wa baraza la nafaka la ukanda wa Afrika Mashariki (EAGC).

Amesema Serikali itaendelea na jukumu la kuhakikisha chakula kinakuwepo nchini.

Waziri amesema mwanzoni mwa mwaka huu baadhi ya wabunge na vyombo vya habari vilimshinikiza atangaze uwepo wa njaa nchini lakini hakufanya hivyo kwa sababu hapakuwa na njaa.

"Siko kwenye nafasi ya kutangaza njaa lakini nisingemshauri Rais kufanya hivyo kwa kuwa licha ya mavuno kidogo yaliyokuwepo kipindi kile, Serikali inaamini watu walikuwa na chakula cha kutosha," amesema Dk Tizeba.

Amesema hata yeye angekuwa Rais asingeweza kutangaza njaa kwa kuwa hali hiyo ilitokea ikiwa ni miezi miwili tu tangu wafanyabiashara waishinikize Serikali kutoa vibali vya kuuza nafaka nje ya nchi.

"Isingewezekana njaa kuja ghafla. Kitendo cha wafanyabiashara kutaka ruksa ya kuuza mazao nje kilimaanisha chakula kilikuwepo cha ziada," amesema Dk Tizeba.

Hata hivyo, Dk Tizeba amesema hali ya chakula kwa mwaka huu imepungua kwa asilimia tatu kulinganisha na mwaka jana.

Kutokana na hilo, amesema chakula kinapaswa kutumika vizuri kuepuka upungufu.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: