
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imepokea madaktari 16 kutoka Cuba wenye utaalamu wa aina tofauti ambao watafanya kazi ya kutoa huduma ya afya na kufundisha Muhimbili kwa miaka miwili.
Miongoni mwa wataalamu hao wamo madaktari bingwa wawili wa usingizi, madaktari bingwa wawili wa wodi za wagonjwa mahututi, daktari bingwa wa Radiologia, daktari bingwa wa upasuaji wa macho na wauguzi kumi wa vyumba vya wagonjwa mahututi.
Akiwapokea jana kwa niaba ya serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya, alisema watasaidiana na wa Kitanzania kutoa huduma bora zaidi zikiwamo zile zilizohitaji utaalamu wa nje ya nchi.
Dk. Ulisubisya alisema wataalamu hao kwa kipindi chote watakachokuwapo Muhimbili, watawafundisha wataalamu wa Kitanzania ili kuongeza kasi ya utoaji huduma za kibingwa katika ubora wa kimataifa.
“Ujio wenu hapa Tanzania utatupunguzia aina ya wagonjwa kwenda nje ya nchi kutafuta tiba zaidi, tunaamini kwa kipindi cha miaka miwili mtakachokaa hapa mkiondoka mtaacha mabaki ya ujuzi weledi na utendaji kazi uliotukuka,” alisema.
Pia alisema ujio wao unatokana na mahusiano kati ya Tanzania na Cuba yaliyojengwa na waasisi wa mataifa hayo.
“Mwanzilishi wa taifa la Cuba aliwahi kusema hawatoi mabaki waliyonayo bali wanatoa walichonacho, tumefarijika kwa ujio wenu,” alisema.
Pia alisema Muhimbili imeboreshwa kimiundombinu na huduma mbalimbali zinazotolewa hapo zimeongezeka.
“Tunaupongeza uongozi wa hospitali ambao umekuwa ukiboresha huduma kila mara, kuwapata wataalamu wengi na kwa wakati mmoja ni shughuli iliyofanywa na uongozi wa Muhimbili, tunaupongeza kwa kazi hii waliyofanya baada ya kwenda Cuba kuwaeleza changamoto tulizonazo,” alisema.
Dk. Ulisubisya alizitaka taasisi nyingine ziige kilichofanywa na MNH ili kupunguza utegemezi kwa Serikali Kuu.
Alisema uhusiano kati ya nchi hizo umelenga kila baada ya muda fulani wanatoa wataalamu kwenda hospitali mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru, alisema katika dhamira ya kutoa huduma za kibingwa ambayo inaendana na kuitikia wito wa Serikali, wamekarabati na kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 13 hadi kufika 20.
Pia alisema wameondoa changamoto ambayo ilikuwa inasababisha wagonjwa wanaohitaji huduma ya upasuaji kusubiri kwa muda mrefu.
“Tumeongeza wodi za wagonjwa mahututi ili kutekeleza azimio la Shirika la Afya Duniani (WHO) linaloelekeza kuwa na asilimia 10 ya vitanda katika hospitali. Muhimbili inatakiwa kuwa na vitanda 150 kwa hiyo tumeviongeza kutoka 21 hadi kufikia 88,” alisema.
Kuhusu rasilimali watu hasa wodi ya wagonjwa mahututi na idara ya utoaji dawa za usingizi, Prof. Museru alisema wamekuwa wakigharamia mafunzo ya muda mfupi kwao.
Alisema wauguzi 20 wamenufaika na mafunzo hayo ya muda mfupi nchini India.
“Kutokana na uhaba wa wataalamu tulionao, tulipeleka maombi yetu Cuba leo tumepokea wataalamu hawa 16 watakaotusaidia kuziba pengo hilo kwa muda,” alisema.
Alisema wataalamu hao watasaidia kulingana na utaalamu wao wakati mipango ya kusomesha wataalamu wa Tanzania inafanywa.
Mwakilishi wa Balozi wa Cuba nchini, Dk. Moylen Zequeira, alisema mkataba wa kubadilishana wataalamu utachangia kubadilishana uzoefu kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya afya.
Tanzania imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa madaktari bingwa, hivyo ujio huo utasaidia kwa kiasi fulani kupunguiza changamoto hiyo.
Mei 3, mwaka huu, akinukuu ripoti ya Madaktari Wenza wa Afrika (Africa Cuamm) ya mwaka jana, Waziri Kivuli wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Godwin Mollel, aliliambia Bunge kuwa asilimia 74 ya madaktari nchini wanaishi mjini na daktari mmoja anahudumia wagonjwa 78,880 kwa maeneo ya vijijini, kinyume cha maelekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) linalotaka daktari mmoja ahudumie wagonjwa elfu moja (1:1,000).
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa Oktoba 2016, Tanzania ina upungufu wa madktari bingwa kwa asilimia 58.1.
Post A Comment: