Chama cha Demakrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka serikali kuweka wazi utaratibu unaosemwa ulifuatwa na CCM kufanya mkutano wao wa chama Ikulu jijini Dar es salaam, ili kila mmoja ajue iwapo atahitaji kwenda kufanya mkutano hapo.


Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA bwana John Mrema, amesema kama ukumbi wa Ikulu unaruhusiwa kufanyika mkutano na mtu yeyote, basi waweke wazi utaratibu na bei ili wengine nao wakiwa na vikao vyao wasisite kwenda ili kuongeza pato la taifa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: