Mkazi wa Mtaa wa Mitandi Lindi Mjini, Mussa Hassan (35) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kulipa fidia ya Sh1 milioni, baada ya kukutwa na makosa ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa miaka 13 aliyekuwa anasoma darasa la sita.


Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa, Erasto Philly alisema Mahakama imemtia hatiani mshtakiwa kutokana na ushahidi uliotolewa na shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mwanafunzi.

Hakimu Philly alisema mshtakiwa alitenda makosa hayo Agosti 2017, kwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi huyo.

Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Emmanuel John aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kutokana na mshtakiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake ikilinganishwa na wa binti
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: