KOCHA msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema kuwa watahakikisha wanamaliza hasira zao za kutoka sare na Lipuli kwenye mchezo wao dhidi ya Njombe Mji.


Yanga itaumana na Njombe Mji Septemba sita kwenye Uwanja wa sabasaba mjini Njombe ukiwa ni mchezo wa pili wa msimu huu.

Akizungumza na gazeti la  Nipashe jana, Nsajigwa, alisema kuwa matokeo dhidi ya Lipuli yamewanyong’onyesha mashabiki wao na sasa wanataka kuwarudishia furaha yao.

Alisema kuwa wanajiandaa kupambana na hali yoyote watakayokutana nayo Njombe kwenye mchezo huo wa ligi Kuu Tanzania Bara.

“Tunaenda huku tukiwa na matokeo ambayo hayajatufurahisha, kwa namna yoyote tutakayopambana nayo tutahakikisha tunapata ushindi ili kurudisha furaha ya mashabiki wetu,” alisema Nsajigwa.

Aidha, nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema kuwa mashabiki wa timu hiyo wasubiri kuona kile watakachokifanya kwenye mchezo huo wa ugenini.

“Kikubwa mashabiki waendelee kuwa na imani na sisi, matokeo ya sare na Lipuli wala yasiwaumize, tutarudi kwenye mstari wetu kuanzia mchezo ujao (dhidi ya Njombe Mji),” alisema Cannavaro.

Alisema kikosi chao kinazidi kuimarika baada ya mshambuliaji Obbrey Chirwa kuruhusiwa kucheza na TFF baada ya kuona hana hatia kufuatia vurugu mchezo wa mwisho wa ligi kuu msimu uliopita dhidi ya Mbao FC.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: