Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema kuwa anafahamu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anayo mengi ya kuzungumza juu ya tukio la kupigwa risasi kwani gari lililotumika na washambuliaji ndilo gari ambalo baadhi ya wabunge walidai linawafuatilia. 


"Hii gari imeripotiwa kufuatilia wabunge kadhaa hapa nikiwepo mimi, na tulisha ripoti gari hilo kwamba hatuelewi ni mtu gani ambaye anatufuatiliaga. sasa gari hiyo hiyo namba hizo hizo na idadi ya watu hao hao lakini hatua hazikuchukuliwa mpaka maswahibu yamemkuta mwenzetu ni wazi hili jambo ni kubwa na najua Lissu anayo mengi ya kutuambia". Nape

Nape amesema ingawa vyombo vya dola vitaendelea na kazi ya upelelezi lakini angependa kama Lissu akirudi kutoka kwenye matibabu azungumzie zaidi kwani hata siku alipozungumza na wanahabari kuhusu gari linalomfuatilia hakusema kwa undani.

"Mh. Lissu pamoja na dereva wake ninauhakika wana mengi ya kusimulia juu ya hili kwani tangu amelilalamikia siyo muda mrefu kutoka sasa. Na kwa vile tayari amejeruhiwa anaweza akatueleza kwa kina juu ya tukio hili" Nape .
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: