Winga wa timu ya Taifa Simon Happygod Msuva amefunguka na kusema hatua ya yeye kufikia kuchezea nje ya nchi ni kutokana na Wivu wa kimaendeleo alioupata kutoka kwa mchezaji mwenzake Mbwana Ally Samatta anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji.


Msuva amefunguka hayo mara baada ya kupachika mabao mawili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana ambapo amedai kuwa wakati Samatta alivyoanza kucheza nje alimvutia kiasi cha yeye kufanya bidii ili aweze kutoka kama mwenzake.

“Samatta ametuonesha mfano flani sisi wachezaji wa nyumbani kwa upande wangu nimefurahi Samatta kuonesha njia wengine tunafuata na tumemfuata Samatta kwa wivu wa kimaendeleo, kwa nini yeye anafanya vizuri nje lakini wakati mwingine  Samatta huwa anatuambia kila mchezaji una uwezo hiyo ilikuwa ikitupatia wivu," Msuva.

Msuva ameongeza kuwa, “Namshukuru Mungu kwa hatua niliyopiga na nafurahi kurudi nyumbani kulitumikia Taifa langu kwa sababu nimetoka Tanzania na nimepata timu Morocco, kiukweli nje ni nje tukiangalia mfano Samatta ametoka wakati ambao kulikuwa hakuna mchezaji anacheza nje” 

Pamoja na hayo Msuva ameongeza kuwa yeye kufunga katika mechi ya jana kutamuongezea nafasi nzuri ikiwemo uaminifu katika timu yake ya huko nje ya Nchi.

Unapofunga kwenye nchi yako, kwenye timu za nje wanaongeza uaminifu kwako. Hivyo naamini kwa nilichofanya leo kitanipa nafasi nzuri kwenye timu yangu ya Morocco. Pia niwatie moyo wachezaji wenzangu wanaochezea hapa nyumbani kwamba kila mmoja anauwezo wa kwenda kucheza nje ya nchi hivyo wasikate tamaa na wazidi kujituma. Msuva aliongeza.

Mechi ya jana Septemba 2 ndiyo ilikuwa ya kwanza kwa Msuva kucheza nyumbani baada ya kusaini kuchezea timu ya Difaa El Jadid ya Morocco.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: