
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
WATANI wa jadi nchini, Yanga na Simba wanatarajia kupimana tena viwango vyao katika mechi ya mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu 2017/18 Oktoba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki mbili mbele kutoka tarehe ya awali iliyokuwa imetangazwa, imefahamika.
Mechi hiyo itakuwa ni ya pili msimu huu baada ya timu hizo kukutaka Agosti 23, mwaka huu katika mechi ya ufunguzi ya kuwania Ngao ya Jamii ambapo mabingwa wa Kombe la FA, Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa penalti 5-4 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare tasa.
Moja kati ya mambo yanayovutia mashabiki wengi katika mchezo huo ni pamoja na kuona kama kiungo mpya wa Yanga, Papy Tshishimbi, ataweza kuonyesha kiwango cha juu kama alivyofanya kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, huku straika wa Simba, Emmanuel Okwi, naye akitazamwa kama atawekewa ngumu tena kuziona nyavu kama ilivyo kuwa kwenye mechi hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa awali, timu hizo zilikuwa zikutane Oktoba 14, mwaka huu, lakini jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa ratiba mpya na sasa zitakutana wiki mbili mbele huku ikionyesha kuwa mchezo wa marudiano ambao utakuwa ni wa raundi ya 23, utafanyika Machi mwakani katika tarehe ambayo haijawekwa wazi.
Ratiba hiyo ambayo imefanyiwa marekebisho kwa kuzingatia Kalenda ya Fifa na mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Shirikisho Afrika na Kombe la Mapinduzi, inaonyesha kuwa ligi hiyo itaendelea Jumamosi kwa Azam kuikaribisha Simba na Jumapili Yanga itakuwa ugenini ikicheza na Njombe Mji.
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watashuka tena uwanjani Septemba 16 kuwavaa wenyeji Majimaji ya Songea wakati siku inayofuata Simba wataikaribisha Mwadui FC kwenye Uwanja wa Uhuru jijini.
Ligi hiyo inayotoa mwakilishi wa Tanzania Bara kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, inatarajiwa kumalizika ifikapo Mei 26, mwakani na kufuatiwa na mchezo wa fainali ya mashindano ya Kombe la FA ambayo bingwa wake atapeperusha bendera ya nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mechi nyingine ambazo hazijapangiwa terehe kutokana na kusubiri kalenda ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho ni kati ya Ndanda dhidi ya Yanga, Simba vs Mbao, Mtibwa Sugar vs Yanga, Simba vs Stand United, Yanga vs Stand United na Njombe Mji dhidi ya Simba.
Ratiba hiyo pia inaonyesha kipindi cha dirisha dogo la usajili kitakuwa kati ya Novemba 15 hadi Desemba 15, mwaka huu.
Post A Comment: