MBUNGE wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu, amesema Tanzania kwa sasa inahitaji Katiba Mpya na kushauri mihimili mitatu ya utawala iwe na mipaka.


Mihimili mitatu ya dola ni Serikali, Bunge na Mahakama ambayo kila mmoja una mamlaka yake katika utendaji na haiingiliani.

Mihimili hiyo kila mmoja una majukumu yake yaliyoainishwa vizuri kikatiba, ili kuhakikisha hakuna mwingiliano baina ya mmoja na mwingine kwa lengo la kuifanya iwe huru katika utendaji wao.

Juzi, katika ukurasa wake wa Twitter, Nyalandu alisema Tanzania inahitaji katiba mpya na kwamba mihimili ya utendaji wake iwekewe mipaka iliyo wazi.

“Tanzania inahitaji Katiba mpya… na kuwapo ‘checks and balances’ (uangalizi na usawa) kwa Serikali, Bunge na Mahakama,” alisema Nyalandu.

Mchakato wa kupata katiba mpya ulianza Aprili, 2012 baada ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete kuwateua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walioongozwa na Jaji Joseph Warioba na makamu wake, Jaji Augustino Ramadhan.

Baada ya kukusanya maoni, Tume hiyo Machi 18, 2014 kupitia kwa Jaji Warioba iliwasilisha kwenye Bunge Maalum la Katiba.

Hatua iliyofuata ilikuwa kujadiliwa na Bunge, ili kuandika Katiba Mpya Inayopendekezwa na kazi hiyo ilifanyika na kukabidhiwa kwa Rais, lakini hadi sasa hakuna kilichoendelea baada ya hapo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: