
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MTU mmoja, Imma Habibu, mkazi wa kijiji cha Vilabwa, Kisarawe mkoani Pwani ameuawa na kaka yake, Ramadhani Habibu, kwa kuchomwa kisu baada ya kutokea mabishano kati yao kuhusu ukubwa wa makalio ya mwanamke mpita njia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi Jonathan Shanna, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Ramadhani (23) amekiri mbele ya polisi kumuua Imma (26) kwa kumchoma kisu upande wa kulia kifuani.
Kamishna Shanna alisema Ramadhani aliuawa juzi majira ya saa mbili asubuhi alipokuwa kijiweni na wenzake.
Alisema wakiwa kijiweni hapo, ulitokea ugomvi kati ya Ramadhani na kaka yake Ramadhani, baada ya mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuwa na maumbile makubwa kwenye makalio, kupita mbele yao.
Alisema baada ya mwanamke huyo kupita, yalizuka mabishano na Imma alisema yalikuwa makubwa huku Ramadhani akisema ni ya kawaida na si makubwa.
Kamanda Shanna alisema katika mabishano hayo, ndipo ulipozuka ugomvi hadi kufikia hatua ya Ramadhani kumuua kaka yake kwa kumchoma kisu kifuani upande wa kulia na kufariki dunia akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Kisarawe.
Alisema Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa kufanya mauaji hayo na kwamba atafikishwa kortini mara moja kwa kuwa amekiri kuhusika.
Wakati huo huo, Kamanda Shanna ametoa onyo kwa wananchi wenye tabia za udhalilishaji kwa wanawake kuiacha mara moja.
Kamanda Shanna alisema vijana wanaoshinda vijiweni wanapaswa kuacha tabia ya udhalilishaji, hasa kwa wanawake, kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Alitaka mtu yeyote aliyefanyiwa vitendo vya namna hiyo kutoa taarifa polisi, ili wahusika waweze kufikishwa mahakamani.
"Wito wangu kwa wananchi wote wanaokiuka haki za binadamu, kwa kudhalilisha wengine, hususani wanawake, kuacha mara moja," alisema Kamishna Shanna.
"Vitendo vyovyote vinavyoashiria udhalilishaji ama kwa kukonyeza au kutumia lugha za kebehi ni kosa kisheria, tutawachukulia hatua."
Aidha, Kamanda Shanna alitoa rai kwa wanawake kuvaa nguo zinazositiri maungo yao, ili kuepusha vishawishi na matamanio kwa wanaume.
Mauaji ya Imma Habibu yanafanana na tukio la binti mwenye umri wa miaka 19, Rukia Ally aliyedaiwa kumuua kwa kumchoma kisu kaka yake wa kuzaliwa, Said Ally, Januari 24, 2015 Tegeta Mivumoni, Dar es Salaam.
Ilidaiwa kuwa binti huyo alimchoma kaka yake kwa kisu baada ya marehemu kutaka kudhibiti tabia zisizofaa za dada yake, ikiwamo matembezi ya usiku.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo, msichana huyo hakuwa amerudi nyumbani kwa siku tatu, hivyo aliporejea saa tatu usiku, kaka yake alimuuliza alikokuwa, lakini alishindwa kutoa majibu ya kueleweka.
Ndipo kaka huyo alimchapa kwa fimbo mguuni kama ishara ya kumkanya, lakini ghafla Rukia alichomoa kisu alichokuwanacho nguoni mwake na kumchoma nacho Said upande wa kushoto wa kifua.
Credit - Nipashe
Post A Comment: