
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MFANYABIASHARA Yusufually Manji, ambaye mapema wiki hii alivuliwa udiwani, amepinga kitendo hicho na kuomba Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuiandikia barua Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuwa ameshindwa kuhudhuria vikao kwa sababu ni mtuhumiwa na yuko mahabusu kwa miezi miwili sasa.
Kadhalika, ameiomba mahakama kumwelekeza DPP aiandikie barua halmashauri hiyo sababu za kutohudhuria vikao, sababu ambazo zimeelezwa chanzo cha kuvuliwa kwake udiwani, kwa kuwa ana kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Manji alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, kwamba amesoma kwenye gazeti kuwa amevuliwa udiwani wa Kata ya Mbagala Kuu kwa kutokuhudhuria vikao.
"Mheshimiwa mimi niko mahakamani kwa zaidi ya miezi miwili sasa na bado niko mahabusu. Nimesoma kwenye gazeti kwamba nimevuliwa udiwani wangu, sitambui najua mimi bado ni diwani" alidai na kuongeza:
"Namwomba DPP aiandikie barua halmashauri hiyo kwamba niko mahabusu, nimetumia zaidi ya Sh. milioni 70 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wangu wa Mbagala Kuu na si mfuko wa halmashauri hiyo kwa hiyo sitambui kuvuliwa nafasi hiyo."
Kutokana na maombi hayo, Hakimu Shaidi alisema amesikia hoja zake na alipanga kesi hiyo kutajwa Septemba 18, mwaka huu.
Awali kabla Manji hajapewa nafasi ya kuwasilisha hoja zake, upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na uliomba tarehe ya kutajwa.
Manji na wenzake wanatuhumiwa kukutwa na mihuri ya mbalimbali ya JWTZ isivyo halali, vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 236.5.
Mbali na Manji, washtakiwa wengine kuwa ni Ofisa Rasilimali Watu Deogratius Kisinda (28), Mtunza Stoo, Abdallah Sangey (46) na Mtunza Stoo Msaidizi, Thobias Fwele (43).
Ilidaiwa katika shtaka la kwanza kuwa Juni 30, mwaka huu eneo la Chang'ombe, Temeke jijini Dar es Salaam, Manji na wenzake walikutwa na polisi wakiwa na Mabunda (majola) 35 ya vitambaa vya kutengezea sare za JWTZ zenye thamani ya Sh. milioni 192.5 na kwamba zilipatikana isivyo halali.
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa alikutwa Julai Mosi, katika eneo la Chang'ombe 'A', Temeke jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walikutwa na mabando manane ya sare za JWTZ zenye thamani ya Sh. milioni 44.
Upande huo wa Jamhuri uliendelea kudai kuwa, Juni 30, la tukio la kwanza, washtakiwa walikutwa na muhuri wa JWTZ uliokuwa na maandishi 'Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha Jeshi JWTZ' bila kuwa na uhalali kitendo ambacho kinahatarisha usalama wa nchi.
Aidha, siku ya tukio la tatu, washtakiwa wote kwa pamoja walikuwa na muhuri wenye maandishi "Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupora Dodoma" bila uhalali kitendo ambacho kinahatarisha usalama wa nchi.
Shtaka la tano, siku ya tukio la tatu na la nne, Manji alikutwa na muhuri wenye maandishi "Comanding Officer 835 KJ Mgambo P.O BOX 224 Korogwe" bila kuwa na uhalali kitendo ambacho kinahatarisha usalama wa nchi.
Ilidaiwa katika shtaka la sita, Julai Mosi, mwaka huu eneo la Chang'ombe 'A', washtakiwa wote walikutwa na namba za gari zenye usajili wa SU 383 iliyopatikana isivyo halali na pia walikutwa na namba ya gari SM 8573 iliyopatikana isivyo halali.
Kwa mujibu wa mashtaka hayo yaliyofunguliwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa taifa, washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao.
Post A Comment: