Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo Zitto Ruyagwa Kabwe ameungana na kauli iliyotolewa leo na Baraza la Vijana la CHADEMA kuitaka serikali kutia uzito uchunguzi wa jaribio la kuuliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusu vyombo vya kimataifa.


Kwenye ukurasa wake wa twitter Zitto Kabwe amendika ujumbe akivitaka vyombo vingine vya kimataifa kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu, kwani haviamini vyombo vya ndani.

"Natafuta uchunguzi wa kujitegemea kimataifa juu ya jaribio la mauaji dhidi ya Mbunge Tundu Lissu, vyombo vya ndani sio vya kuviamini", aliandika Zitto Kabwe.

Zitto Kabwe aliendelea kwa kuandika kwamba watu waliofanya tukio hilo wana lengo la kuwafunga midomo wanapopaza sauti zao kupinga uonevu, hivyo hawatakiwi kukaa kimya kwani watakuwa wamewapa ushindi.

Jana asubuhi Baraza la Vijana CHADEMA limefanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia tukio la kupigwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu, na kuitaka serikali itie uzito jambo hilo kwa kuunda tume huru maalum ya kuchuguza, pamoja na vyombo vya kimataifa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: