
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya viwanda katika maeneo yao kwani vitasaidia katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana.
Waziri Mkuu alipozungumza na watendaji na wananchi wa mkoa wa Morogoro amesema mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda ambao unalenga kuinua uchumi wa Taifa kutoka wa chini kwenda uchumi wa kati, hivyo ni muhimu kuvifuatilia.
βViwanda hivi vinatupa uhakika wa ajira nchini kwa vijana kwa sababu vinauwezo wa kuajiri watu wengi na wa kada mbalimbali, hivyo ni muhimu tukafuatilia utendaji wake. Lakini mbali na kutoa ajira nyingi, pia viwanda vitawezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao na kukifanya kilimo kuwa na tija," Mhe. Majaliwa.
Pamoja na hayo Majaliwa ameongeza na kusema kwamba muda mrefu sekta ya viwanda nchini ilikuwa haifanyi vizuri jambo ambalo lilisababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa soko.
Hata hivyo Waziri Mkuu amesisitiza uaminifu kwa wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda mbalimbali kuwa waaminifu ili kuviwezesha viwanda hivyo kuendelea na uzalishaji.
Post A Comment: