INAJULIKANA kiafya kuwa, uvutaji sigara ni kukaribisha kifo. Linapokuja suala la kuacha uvutaji, sio jambo rahisi kama watu wengi wanavyofikiri. Je, njia gani bora za kumfanya mtu aache kuvuta sigara?


Ni kazi ngumu kidogo kuacha uvutaji wa sigara. Uvutaji ni tishio kwa maisha yetu. Yawezekana hufahamu kwamba nusu ya watu wanaovuta sigara watakufa, ikiwa ni matokeo ya athari kilevi hicho. Sigara inasababisha robo ya vifo vyote vya kansa nchini Uingereza kila mwaka.

Kuacha uvutaji sio jambo rahisi sana. Hii ndiyo sababu kwa nini hadi sasa bado kuna watu milioni 10 wanaovuta sigara nchini Uingereza. Huku watu kati ya milioni tatu hadi nne wanajaribu kuacha wakati wowote bila ya mafanikio.

Mwezi uliopita, ilitangazwa rasmi kuanzishwa Mpango Mpya wa Udhibiti wa Tumbaku, unaolenga kupunguza idadi ya Waingereza wanaovuta sigara ifikapo mwaka 2022.

Njia tofauti zinazowezesha kuacha matumizi ya kilevi hicho ni zifuatazo, kama zinavyotambuliwa kwa majina yafuatayo:
Cold turkey

Hiyo ni mbinu ngumu, lakini yenye ufanisi. Uchunguzi wa hivi karibuni umebainisha kwamba wanaoacha kwa ghafla ni asilimia 25 tu, lakini kuna uwezekano wa kufanikiwa, kuliko wanaojaribu kuacha kwa hatua.

Ikiwa mtu anaamua kutumia njia hiyo, anapaswa achague tarehe mahsusi ya kutekeleza nadhiri yake. Ni vyema akajithibitishia muda maalum, akihakikisha uchaguzi huo wa muda haujajaaa matukio ya kijamii au wakati wa matatizo na pilika katika kazi, ili imfanya asigubikwe na kiu kubwa ya sigara.

Mvutaji anatakiwa aishi na kanuni ya 'angalau mvuto mmoja.' Kwa mujibu wa wataalamu hao, hamu ya kawaida ya sigara inadumu kwa mtu walau kwa takribani dakika tano.

Hivyo, mvutaji anatakiwa kuwa na orodha ya mikakati ndani ya dakika tano hizo kuvuruga hisia, iwapo hamu ya kuvuta itakapomjia.

2. Tembe za kumung’unya(Patches, gum, lozenges)

Kutumia tembe za kumung’unya kwa wiki nane yaweza kuongezea mara mbili nafasi ya kuacha sigara. Itapunguzia tamaa ya kuvuta sigara, bila ya kuharibu afya binafsi. Inafanya kazi kwa kuchukua nafasi ya nikotini ipatikanayo kutoka kwenye sigara au tumbaku.
Masharti ya tiba

Hali nyingine za matibabu zinahitaji ushauri wa kitaaluma juu ya kutumia tembe za ‘patches’ za nikotini, ‘gum’ na ‘lozenges.’
Pia ni muhimu kuangalia yafuatayo:

• Kama mtu ana mimba au unanyonyesha.

• Iwapo anaugua kisukari.

• Mtu akitumia dawa za afya ya akili.

• Mtumiaji mwenye uzito chini ya kilo 45.

• Kama anasumbuliwa na maradhi ya moyo au kiharusi katika muda usiozidi wiki mbili zilizopita.

Tiba inachukua nafasi ya nikotini kwa kutoa hisia zake kwa njia nyingine, ili kusaidia kuzuia hamu ya sigara.

Uchunguzi unaonyesha kuwa, aina hiyo ya tiba inaongeza uwezekano mara mbili ya mtu kuacha sigara, ingawaje inatahadharishwa kwamba si vyema ikatumika kwa muda mrefu.

3. Sigara ya kielektroniki (Vape)

Watu wengi wamegeukia uamuzi wa kuacha sigara, kwa kuvuta sigara za kielektroniki ambazo kimsingi zimeumbwa mfano wa sigara haliso na zinazopatikana katika aina zote za miundo na ladha. Hivyo, ni rahisi kupata picha, kwa nini Waingereza wapatao milioni 2.9 wanaitumia.

Aina hiyo ya sigara, huifanya mikono ya mvutaji iwe na shughuli ya kufanya kwa kuvuta aina hiyo ya sigara isiyo na majivu na gesi chafu ya ya aina ya carbon monoxide au vingine vinavyopatikana katika sigara halisi.

Hata hivyo, tafiti kadhaa zinaonyesha hewa hiyo inaweza kusababisha mabadiliko ya chembehai zinazoweza kusababisha kansa.

Hayo ni matokeo ya tafiti mpya, ambayo yanaelezwa hayana ushahidi unaojitosheleza , jambo linaloleta hoja nyingine kwamba ‘vape’ inatakiwa kuvutwa kwa tahadhari.

4. Ushawishi kitaalamu (Hypnotism)

Utafiti uliofanywa kwa watu 6,000 wanaovuta sigara, inaonyesha kuwa njia hiyo ina mafanikio makubwa, kwa kuwashawishi wavutaji watambue madhara na faida za kuacha sigara

"Inachukua siku chache tu kwa nikotini kuondoka mwilini mwako. Kwa hiyo, kile unachoachwa nacho ni tamaa ya kisaikolojia," anasema mtaalamu Brian Jacobs, anayesema kinachoshughulikiwa hapo ni tamaa, wakati mtu yupo mapumzikoni.

Baada sigara ya mwisho

Baada ya saa nane, oksijeni hurudi katika hali ya kawaida mwilini na tindikali ya nikotini na hewa ya carbon monoxide hupungua kwa kiwango cha nusu ya kilichokuwapo.

Baada ya saa 48, mwilini mwa binadamu hakuna nikotini inayobaki mwilini na uwezo wa kuonja na harufu unaboreshwa. Hatari ya kuwa na mashambulizi ya moyo, nayo inaanza kupungua.

Hatua inayofuata baada ya kati ya wiki mbili na 12, mzunguko wa damu, hewa, maji na mahitaji mengine mwilini yanaboreka.

Ni hali inayoendelea hata kufika baada ya miezi mitatu hadi tisa, mapafu yanakuwa yameboreka kwa asilimia 10 na kukohoa kunakuwa kumepungua.

Inapofika mwaka mmoja umepita, hatari ya ugonjwa wa moyo kwa mvutaji inakuwa katika kiwango cha nusu ilivyokuwa awali na ikiendelea katika miaka 10 baadaye, hatari ya saratani ya mapafu huwa nusu kwa mvutaji, kulinganisha na alivyokuwa awali.

Ikiendelea baada ya miaka 15, moyo unakuwa salama dhidi ya hatari ya mashambulizi ya sawa na kuwa sawa na asiyetumia sigara.

Simulizi za aliyeacha

Muathirika aliyekutakana na mtaalamu wa tiba hiyo anasimulia:"Kwanza, hypnotherapist (Mtaalamu mshauri) alitumia nusu saa kuzungumza nami kuhusu sababu zangu za kutaka kuacha.

Kabla ya kunishawishi kupitia mbinu za kuvuta ambazo kwa mshangao wangu, alinipeleka katika hali ya karibu ya kuutua mzigo wa uvutaji.

“Zaidi ya dakika 30 zilizofuata, niliongozwa kupitia maonyesho (kutafakari sigara iliyokuwa na uso wa mtu anayechukiza) kisha kuunganishwa kwa maneno yanayokufanya ufurahi."

“Ni wiki tu tangu nianze kufanyiwa hypnosis siwezi kusema kwa hakika kuwa imefanya kazi au la. Lakini shauku yangu ya kuvuta sigara tena inapotea taratibu. "
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: