KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, amemuonya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa kamwe njama anazozifanya haziwezi kukiboa chama hicho.


Akizungumza na wanachama wa chama hicho katika mkutano mkuu wa wilaya ya Magharib A Unguja, Maalim Seif, alisema Msajili badala ya kuvilea vyama vya siasa, amekuwa akivibomoa hasa vile vyenye nguvu kikiwamo chama cha CUF.

β€œNjama anazozifanya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kushirikiana na Profesa Ibrahim Lipumba, kuibomoa CUF, kamwe hawezi wala hatoweza, wanachokifanya ni sawa na kutwanga maji katika kinu,” alisema.

Aidha, alisema njama hizo pia zimekuwa zikiungwa mkono na vyombo vya dola kwa kuwa kila anapoenda Lipumba kukihujumu chama hicho, amekuwa akilindwa na vyombo hivyo.

β€œHuu ni mpango wa dola, Lipumba yupo mbele tu na mimi nawaambieni wajumbe kuwa visa vyao vitazidi kipindi hiki kwa kuwa hivi sasa wana mpango wa kuhujumu matawi ya chama hiki ili wanaCUF waje juu wapate nafasi ya kuwakamata viongozi wa wao wakiamini kufanya hivyo haki haitorudi, lakini pia wana mpango wa kufungua matawi Zanzibar kinyume na utaratibu tuliojiwekea,” alidai.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: