Baada ya kuachia video ya wimbo wake wa ‘I Miss You’ ambayo iliwahi kuvuja muda mrefu kidogo, Msanii wa muziki kutoka 255 Diamond Platnum ameonesha kufurahia views wanaoitazama video hiyo mtandaoni.


Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameonesha wazi wazi furaha hiyo na kuwashukuru mashabiki wake kwa kuitazama video hiyo kwa kuandika “611,054 Views within a Day and few hours….Views Laki sita na kumi ndani ya siku Moja na Masaa….. Eish! Nyie Mafans Mie Nawapenda Ujue jamani😟😢 #IMissYou,”

Hata hivyo ngoma hiyo imezidi kutikisa mtandao wa YouTube kwa kushika video namba moja inayo’trend kwa sasa huku ikiiacha mbali ngoma yake mpya ya ‘Fire’ aliyomshirikisha Tiwa Savage kutokea nchini Nigeria ambayo nayo ilitoka siku moja na ‘I Miss You’
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: