NYOTA wa muziki nchini Uganda, Bebe Cool, baada ya wiki iliyopita kuthibitisha kuwa amepata mtoto wa sita, sasa amesema watoto hao hawatoshi katika maisha yake.


Msanii huyo ambaye alifanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake, Zuena Kirima, kwa miaka 14 iliyopita, amesema lengo lake ni kuwa na familia kubwa na yenye furaha.

β€œNashukuru Mungu kwa kutuongezea ukubwa wa familia yetu, lengo la familia yetu ni kuwa kubwa na tunaamini kwa uwezo wake Mungu tutafanikiwa kama tulivyopanga.

β€œKwa sasa nina jumla ya watoto sita, lakini bado hawanitoshi, natamani kuwa na wengi zaidi ya hapo kwa kuwa napenda sana watoto katika maisha yangu, namuomba Mungu aniwezeshe kupata wengine wengi,” alisema Bebe Cool.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: