Mshambuliaji Danny Welbeck amewaambia Manchester United wamsemehe tu, kwa sababu yupo kazini kwa sasa kuhakikisha Arsenal inakamata nafasi inayostahili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, hivyo hajali machungu anayowapa waajiri wake wa zamani.


Straika huyo, alifunga bao lake la nne msimu huu ambao umekuwa na matatizo mengi ya majeruhi kwa upande wake, lakini bao hilo aliloifunga klabu yake ya zamani ya Man United limeifanya Arsenal kufufua matumaini ya kuifukuzia Top Four ili kukamata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Ushindi huo unaifanya Arsenal sasa kubakiza pointi mbili tu kuiondoa Man United kwenye nafasi ya tatu na kama watashinda mechi yao ya kiporo dhidi ya Southampton kesho Jumatano basi watapanda hadi kwenye nafasi ya tatu na Jose Mourinho na kikosi chake watarudi kwenye nafasi ya sita.

Granit Xhaka, kwa msaada wa mpira wa kuparaza, alifunga bao la kwanza kabla ya Welbeck, ambaye baada ya mechi hiyo alipiga selfie za kutosha na Mesut Ozil kuongeza la pili kwa kichwa, huku akiendeleza kawaida yake ya kuifunga timu yake hiyo iliyomlea tangu utoto wake. Aliwahi kuwafunga pia kwenye mechi ya Kombe la FA uwanjani Old Trafford.

Welbeck anasema hivi: "Kitu muhimu kwetu ni kushinda hasa ukizingatia nafasi tuliyopo kwenye ligi kwa sasa, tunahitaji kuwa juu. Ni nafasi inayohuzunisha, lakini tunajipa matumaini kwamba tutakuwa pazuri mwishoni mwa msimu.

"Kuhusu Man United nimekulia pale, hivyo ni mahali spesho katika maisha yangu, lakini tunapoingia uwanjani ni Biashara nyingine, kwa sababu nitakachofanya ni kuisaidia timu tangu kupata pointi. Unapofunga unafurahi, kuna asiyefurahi. Ni jambo la kawaida."

Katika mchezo huo, kocha Mourinho aliwaanzisha wachezaji wake watatu waliokuwa majeruhi, Chris Smalling, Phil Jones na Juan Mata, ambapo mabeki wa kati walicheza kwa dakika 90 na kiungo Mata alitoka dakika tano kabla ya mechi kumalizika.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: