Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Chamwino, Charles Ulanga ameshangazwa baada ya kutajwa miongoni mwa watu wenye vyeti feki cha kidato cha nne na kuhoji sababu za kutajwa katika orodha ya walioghushi vyeti vya kidato cha nne wakati hajawahi kusoma elimu ya sekondari.


Sakata la Mwenyekiti huyo ni mwendelezo wa utata ulioibuka baada ya ripoti ya matokeo ya uhakiki huo uliobaini wafanyakazi 9,932 wa Serikali na Taasisi zake kuwa na vyeti vya kughushi, kutumia vya watu wengine au cheti kimoja kutumiwa na zaidi ya mtu mmoja.

Ulanga, ambaye pia ni Mratibu wa Elimu wa Kata ya Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, amesema wakati wa uhakiki alipeleka cheti cha darasa la saba na cha ualimu daraja la tatu β€˜A’.

β€œNawashangaa wapi walipopata cheti cha kidato cha nne kwa sababu mimi nilipeleka vyeti viwili; cha darasa la saba na cha ualimu. Sasa hiki cha kidato cha nne walichokikuta feki sijui wamekitoa wapi?” amehoji Ulanga.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: