JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya kundi kubwa la wananchi waliozuia msafara wa Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.


Maelfu ya wananchi hao walitawanywa jana kwa mabomu hayo baada ya kuziba barabara ya Soko la Mbuyuni eneo la Manyema wakati msafara wa Lowassa ukielekea Kata ya Bomambuzi, Manispaa ya Moshi.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basili Lema, alisema polisi walilazimika kurusha mabomu manne ya machozi ili kutawanya umati wa watu waliokuwa na shauku ya kumwona Lowassa.

β€œSaa 10:15 jioni katika Soko la Mbuyuni, polisi walirusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waweze kupisha msafara wa Lowassa kwa kuwa wengi wao waliziba kabisa barabara,” alisema.

Lema alisema kuwa Lowassa aliongozana na wabunge wawili wa chama hicho, Joshua Nasari na Esther Bulaya, kwenda kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo, Ninde Valerian.

Alisema baada ya polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kurusha mabomu hayo, wananchi walitawanyika na kuwezesha msafara huo kupita na kuelekea katika mkutano huo wa kampeni.

β€œBaada ya mabomu kurushwa, wananchi walitawanyika, tukaweza kuelekea katika mkutano wa hadhara na katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi Lowassa alihutubia,” alisema.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah, alithibitisha polisi kurusha mabomu hayo na alisema walifanya hivyo ili kutawanya umati wa wananchi waliokuwa wamefunga barabara katika eneo la Manyema.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: