Magari ya kifahari yameonekana jana katika mazishi ya bilionea Ivan Ssemwanga yaliyofanyika nyumbani kwao Kayunga jijini Kampala.


Ivan aliyekuwa mume wa Zari Hassan maarufu ‘Zarithebosslady’ ambaye kwa sasa ni mpenzi wa Diamond Platnumz, alifariki dunia wiki iliyopita baada ya kupata kiharusi na kuwa katika hali ya koma kwa wiki mbili mfululizo katika hospitali ya Steven Biko huko Pretoria nchini Afrika Kusini.

Gazeti la Uganda, Daily monitor linaripoti kuwa miongoni mwa magari hayo ni pamoja na yale ya marehemu likiwemo Hammer lenye jina la Ivan 9, yale ya vizito mbalimbali wa jiji la Kampala waliohudhuria mazishi hayo pamoja na gari la tajiri wa Tanzania Jack Pemba aina ya Audi lenye jina la A Pemba ambalo lilionekana kuwa la kifahari zaidi.

Katika hali ambayo haikuonekana kuwa ya kushangaza, baadhi ya waombolezaji walionekana wakiomba na kupewa fedha kutoka kwa matajiri mbalimbali waliohudhuria.

Hata hivyo kaburi la Ivan liliwekwa mafungu ya fedha chini ikiwa ni maandalizi ya kuuweka mwili wa bilionea huyo.

Mwili wa Ivan ambao uliwasili Uganda siku mbili zilizopita katika ndege kubwa iliyobeba watu 50, umezikwa katika makaburi ya familia pembeni ya kaburi la baba yake.

Credit - Mwananchi
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: