Tabasamu la kila mmoja kati yetu hutegemea usafi wa kinywa chake unaotokana na kupiga mswaki na kusugua kwa umakini. Changamoto iliyopo ni namna ya kufanya hivyo kwa ufasaha.


Wengi hawafahamu njia sahihi za kupiga mswaki kwa ajili ya afya ya kudumu ya kinywa inayoaanza hapo. Kinywa safi ni msingi wa afya njema ya mwili.

Afya ya kinywa inaanza na meno yaliyo safi. Hili hufanyika kwa kutunza maeneo na meno yanakutana na fizi katika hali ya usafi huzuia magonjwa ya fizi na kuzuia kutoboka kwa meno.

Kufanikisha usafi wa kinywa na meno, kila mmoja anapaswa kuzingatia upigaji sahihi wa mswaki kila siku au inapohitajika. Yapo mambo mengi ya kuzingatia wakati wa kupiga mswaki lakini nitaeleza matano kwa leo.

Kwa afya njema ya kinywa chako, unashauriwa kupiga mswaki mara mbili kwa siku. Wakati unafanya hivyo, usiwe na haraka. Chukua muda wa kutosha kusugua meno yako yote kwa ukamilifu huku ukihakikisha kila kinachopaswa kuondolewa kimefikiwa.

Kulingana na umri, mazingira au hali ya afya, unashauriwa kutumia mswaki sahihi utakaokufaa pamoja na dawa ya meno iliyo na madini ya floridi. Mswaki mzuri ni ule ambao visafishio vyake havikuumizi na unaokaa vizuri kinywani.
Watoto wapewe mswaki unaofanana na umri wao ili kufanikisha hili. Wale wadogo wasimamiwe ili kuzingatia namna ya upigaji na kuepuka kutomeza dawa ya meno ambayo haipaswi kumezwa.


Kanuni ya tatu ni kujizoeza njia nzuri za kupiga mswaki. Unapaswa kuushika mswaki wako kwa namna ambayo visafishio (brashi) vyake vitalenga kwenye makutano ya meno na ufizi.

Unachotakiwa kufanya ni kusafisha meno yako kwa mwendo mfupi wa kwenda mbele na nyuma, juu na chini. Kumbuka kusafisha nje, ndani na sehemu za kutafunia. Halikadhalika usisahau kusafisha ulimi kwa kutumia mswaki wakati ukipiga mswaki.

Ni muhimu kuutunza mswaki katika hali ya usafi kila baada ya kuutumia. Mara zote safisha mswaki wako kwa maji safi umalizapo kuutumia. Unapouhifadhi, usimamishe ili ukauke mpaka utakapoutumia tena.

Kama una miswaki kadhaa na yote unaitunza mahali pamoja, tenganisha huu uliotumia sasa na hiyo mingine ili kuzuia maambukizi ya bakteria. Weka mswaki wako mahali penye hewa ya kutosha vinginevyo huweza kuchochea ukuaji wa bakteria na fangasi kwenye mswaki wako ambao wanaweza kukusababishia maambukizi ya mgonjwa ya kinywa au mwili kwa ujumla.

Kanuni ya tano na mwisho kwa leo ni kutambua wakati sahihi wa kubadilisha mswaki wako. Mswaki hupoteza ubora wake kadri uutumiavyo hivyo kustahili kubadilishwa. Kila mtengenezaji anapaswa kuandika mswaki unaoununua unastahili kutumika kwa muda gani…ingawa hufanya hivyo ila wengi hatuzingatii kusoma maelekezo yaliyomo. Lakini ipo kanuni ya jumla. Unatakiwa kuhakikisha unatumia mswaki mpya kila baada ya miezi matatu mpaka minne. Ni vyema kama utafanya hivyo chini ya muda huo au pale utakapoona umeanza kuharibika.

Flosi

Flosi ni uzi maalumu uliotengenezwa ili kusafisha katikati ya meno ambamo brashi za mswaki haziwezi kufika na kutekeleza lengo hilo. Hivyo, kuflosi ni kusafisha maeneo yaliyo kati ya jino na jino ambayo hayawezi kufikiwa na mswaki.

Kutokana na ugumu wa kupiga mswaki maeneno ya kati jino na jino, inashauriwa kusafisha mara moja kwa siku ili kuimarisha usafi kamili wa kinywa na kujihakikishia siha njema.

Zipo kanuni au taratibu za kuzingatia. Kwanza unashauriwa kukata uzi wa kufanyia flosi wa kutosha. Kwa mtu mzima, inapendekezwa uwe na urefu walau sentimita 45.

Kisha zungusha sehemu kubwa ya uzi huo kwenye kidole cha kati cha mkono mmoja na fanya vivyo hivyo kwenye kidole cha kati cha mkono mwingine.

Flosi hufanywa taratibu. Unashauriwa kuelekeza na kuupitisha uzi kati ya meno ukitumia na kusugua. Sugua meno na sio ufizi. Fanya hivyo kutoka jino moja kwenda jingine kwa zamu.

Flosi jino moja kwa wakati mmoja. Jiridhishe kwa ukamilifu ulioufanya kwenye jino la kwanza kabla hujahamia la pili. Flosi taratibu kwa kusugua kwenye jino kwa kwenda juu na kushuka chini.

Habari njema ni kwamba hujachelewa kwani ukifanya kazi yako vizuri, haijalishi umeanza lini kupiga mswaki au kuflosi matokeo ni sawasawa. Utakuwa na afya njema na utajiamini popote utakapokuwa.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: