
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
BAADHI ya majengo kama shule, hospitali na mengineyo yaliyoathiriwa
na tetemeko la ardhi mkoani Kagera yameanza kujengwa na kufanyiwa
ukarabati.
Aidha, fedha zote za misaada zinazotolewa na watu mbalimbali wakiwemo
wafadhili kutoka nchi za nje zinawekwa katika akaunti moja na kutumika
baada ya kamati maalumu kupitisha matumizi yake kwa lengo la kuhakikisha
zinatumika vizuri.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu,
Brigedia Jenerali Mbazi Msuya aliyasema hayo hivi karibuni alipozungumza na kueleza kuwa uharibifu uliofanywa na tetemeko hilo ni
mkubwa sana na misaada inayotolewa haiwezi kutosheleza mahitaji.
Brigedia Jenerali Msuya alisema ukarabati wa majengo kama sekondari
ya Ihungo na Nyakato pamoja na nyumba za walimu, umeanza pamoja na
kujenga nyumba za muda za walimu hao wakati ukarabati ukiendelea.
Alisema kinachofanyika ni fedha zote kuwekwa kwenye akaunti moja ya
Maafa Kagera na kuna kamati maalumu inayozitoa na kuzigawa kulingana na
mahitaji ya matumizi.
Alisema kwa wafadhili waliojitokeza kujenga shule kama Ihungo na
nyinginezo ambao ni wawili au watatu wanapeleka maombi katika Kamati ya
Maafa mkoani humo ili kuruhusu fedha hizo nyingine kutumika katika
sehemu nyingine iliyoathirika.
“Uharibifu uliotokea ni mkubwa sana na serikali haina uwezo wa
kumpatia kila mwananchi msaada, bali ni kufanya mambo yanayomgusa kila
mmoja kama ujenzi wa shule, hospitali na zahanati na kuwapatia misaada
mingine ya jumla,” alieleza Mkuu huyo wa Maafa nchini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: