
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
KWA mara ya kwanza katika historia yake, Tanzania inatarajia kumpokea Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco keshokutwa.
Aidha, ziara ya mfalme huyo, mbali na kujikita katika kujenga
diplomasia ya nchi hizo mbili, itatumika pia kuiomba Tanzania kusaidia
kupokewa kwa Morocco katika Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine
Mahiga alisema ugeni huo utakuwa mkubwa na wa aina yake.
“Sababu mbili za ziara hii ya mfalme hapa nchini ni Morocco
ilijiondoa katika Umoja wa Nchi za Afrika miaka 32 iliyopita, lakini
hivi karibuni wanachama walipokea barua kutoka kwa nchi hiyo kutaka
kurudi katika umoja huo, kwa kuja hapa atazungumza na Rais,” alisema
Balozi Mahiga.
Mfalme Mohammed wa VI atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Rais
John Magufuli Ikulu yakifuatiwa na mazungumzo rasmi kati yao na ujumbe
aliofuatana nao.
Balozi Mahiga alisema mfalme huyo atakuja nchini
akitokea Rwanda, na atakuwa na ziara ya kutembelea nchi nyingine Afrika
kuzungumza nao kuhusu kurudi kwake AU.
Alisema ziara hiyo pia itatumika kukuza zaidi uhusiano kati ya
Tanzania na Morocco hususan katika masuala ya kiuchumi na kibiashara kwa
faida ya nchi hizi mbili na watu wake ikizingatiwa nchi hiyo
imefanikiwa sana katika nyanja mbalimbali kama vile miundombinu, afya,
madini na ulinzi.
Waziri huyo alifafanua kuwa ziara rasmi nchini ya mfalme itakuwa
kuanzia Jumapili hadi Oktoba 25, mwaka huu na baada ya hapo atakuwa
likizo kwa siku tano ambapo atatembelea sehemu mbalimbali kama matembezi
binafsi.
Vilevile, alisema Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco atatumia fursa ya
ziara hiyo kutembelea Zanzibar na kukutana na Rais Ali Mohamed Shein na
atatembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA) kwa ajili ya
kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Ziara hiyo ambayo imejikita zaidi katika kukuza ushirikiano wa
kiuchumi na kibiashara, ujio wa mfalme atafuatana na wafanyabiashara
kutoka Morocco ambao watakutana na wafanyabiashara wa nchini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: