NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta ni
miongoni mwa wachezaji 30 waliotangazwa na Shirikisho la Soka la
Afrika(CAF) kuwania tuzo za mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika.
Samatta, ambaye ni mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji wa
ndani kwa msimu uliopita, ameteuliwa kushindania tuzo ya mwanasoka bora
wa mwaka wa Afrika kutokana na kiwango bora anachoonesha akiwa na klabu
ya KRC Genk ya Ubelgiji.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba na TP Mazembe, amekuwa na
mchango mkubwa kwenye timu yake ya KRC Genk ambapo aliifungia timu hiyo
mabao muhimu yaliyoiwezesha kuingia kwenye mechi za mchujo za mashindano
ya Europa na kisha kuiwezesha kufuzu kuingia kwenye hatua ya makundi ya
mashindano hayo.
Kwa mujibu wa mtandao wa CAF jana, Samatta anaungana na wachezaji
wengine wawili kutoka Afrika Mashariki kuwania tuzo hiyo wachezaji hao
ni Victor Wanyama kutoka Kenya anayekipiga kwenye klabu ya Tottenham
Hotspurs ya England na kipa wa kimataifa wa Uganda, Dennis Onyango wa
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Wanyama amekuwa na msimu mzuri kwenye klabu ya Southampton na
kumpatia nafasi ya kusajiliwa kwenye klabu ya Tottenham Hotspurs msimu
huu na Dennis Onyango aliiongoza Uganda kufuzu kwa fainali za mataifa ya
Afrika lakini pia ameiongoza Mamelodi Sundowns kuingia fainali ya Ligi
ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Mbali na Samatta wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo yupo
mwanasoka bora wa msimu uliopita wa Afrika, Pierre Emerick Aubameyang
kutoka Gabon ambae anaichezea Borrusia Dortmund ya Ujerumani, Riyahd
Mahrez (Algeria, Leicester City), Islam Sliman(Algeria, Leicester City).
Orodha kamili ya wanaowania tuzo hiyo ni Riyad Mahrez (Algeria,
Leicester City) El Arabi Hillel Soudani (Algeria, Dinamo Zagreb), Islam
Slimani (Algeria , Leicester City) Samuel Eto’o (Cameroon, Antalyaspor),
Benjamin Mounkandjo (Cameroon na Lorient).
Serge Aurier (Ivory Coast, PSG), Eric Bailly (Ivory Coast, Manchester
City), Yao Kouasi Gervais ‘Gervinho’ (Ivory Coast, Hebei Fortune),
Mohamed Salah (Misri, Roma), Mohamed El Neny (Misri, Arsenal), Pierre
Emerick Aubameyang (Gabon, Dortmund).
Andre Ayew (Ghana, West Ham), Victor Wanyama (Kenya, Tottenham),
William Jebor (Liberia, Wydad Athletic Club), Mehdi Benatia (Morocco
& Juventus), Hakim Ziyech (Morocco, Ajax), John Mikel Obi (Nigeria,
Chelsea), Kelechi Iheanacho (Nigeria, Manchester City), Ahmed Musa
(Nigeria , Leicester City).
Cedric Bakambu (DR Congo, Villareal), Yannick Bolasie (DR Congo,
Everton), Sadio Mane (Senegal, Liverpool) , Kalidou Koulibaly (Senegal,
Napoli), Keegan Dolly (Afrika Kusini & Mamelodi Sundowns), Itumeleng
Khune (Afrika Kusini, Kaizer Chiefs).
Mbwana Samatta (Tanzania, Genk), Aymen Abdennour Tunisia, Valencia),
Wahbi Khazri (Tunisia, Sunderland), Dennis Onyango (Uganda, Mamelodi
Sundowns), Khama Billiat (Zimbabwe, Mamelodi Sundowns).
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: