Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Gelacius Byakanwa amedaiwa kuibiwa televisheni ya bapa (flat screen) yenye thamani ya Sh1.5 milioni.


Hata hivyo, tukio hilo limegubikwa na utata baada ya mkuu huyo wa wilaya kukana kuibiwa, lakini mlinzi wake ameandikiwa barua ya kujieleza kutokana na tukio hilo.

Byakanwa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, amehoji ni nani aliyeripoti polisi akisisitiza kuwa hakuna tukio kama hilo. “Mimi sina taarifa labda kama OCD (mkuu wa polisi wa wilaya) amekuambia. Nani aliripoti? Mie sina taarifa,”amesema.

Katibu Tawala (Das) wa wilaya hiyo kupitia barua yake ya Oktoba 17, anathibitisha kutokea kwa wizi huo Oktoba 7.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alipotafutwa alisema alikuwa ametingwa na shughuli muhimu na kwamba, akikamilisha atalizungumzia suala hilo.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: