Pamoja na kuibuka na kushikilia msimamo kuwa anapinga suala la klabu ya Yanga kukodishwa kwa miaka 10 kwa kampuni ya Yanga Yetu Ltd, taarifa zinaeleza Ibrahim Akilimali si mwanachama wa Yanga.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zinaeleza Akilimali ambaye ni katibu wa baraza la wazee wa Yanga, si mwanachama kwa kuwa hajalipa ada kwa zaidi ya miezi miaka sasa.

“Ni kweli, mara ya mwisho alilipiwa na Mwenyekiti (Manji), baada ya hapo hajawahi kulipa ada hata mara moja. Kwa mujibu wa katiba ya Yanga, yeye si mwanachama wa Yanga,” alisema mmoja wa wapasha habari.

Juhudi za kumsaka Akilimali zilifanyika, alipopokea simu akasema: “Nani kakuambia, mbona mnanifuatafuata hivyo, tafadhari mniache, nisipokuwa mwanachama, halafu?” Baada ya hapo alikata simu na ikawa haipatikani.

Akilimali amekuwa mstari wa mbele kuweka msimamo wake kwamba Yanga isikodishwe lakini kumekuwa na barua zinazosamabazwa mitandaoni zikionyesha Akilimali akiweka msisitizo katika suala la Yanga kuwa kampuni.
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: