Na Thabit Karim Muqbell

1: Inasemakana kuna MBU zaidi ya Trilioni 100 Duniani kote. ambao wamegawanyika katika makundi 3,450. Idadi hii ni mara 133 ya watu wote Duniani. 


2: MBU jike huishi takriban miezi miwili wakati dume huishi kwa siku 10 pekee. Baadhi ya majike huishi kwa miezi 6 hii ni kutokana na kuzimia kwa muda kwa sababu ya hali ya ubaridi katika eneo hilo, hali ya joto ikiongezeka basi hufufuka na kuendelea kuishi tena. Jike hutaga mayai kila baada ya siku tatu katika maisha yake yote.

3: Chakula kikuu cha MBU ni matunda na majimaji ya mimea na si damu kama watu wengi wanavyojua. MBU wanaonyonya damu huwa ni jike na ni kwa ajili ya kurutubisha mayai yanayohitaji protein inayopatikana katika damu ya binadamu. MBU dume huwa hanyonyi damu.

4: MBU wakati wa kuuma huingiza kwanza mate katika mwili wa mwanadamu kupitia mrija wake mrefu, mate hayo huwa na "anticoagulant" ambayo hufanya damu kutoka kwa mwanadamu na kuingia mwilini kwa urahisi na hapa ndipo anapoeneza malaria.

5: MBU ndio kiumbe kinachoongoza kuuwa wanadamu duniani kote kuliko kiumbe chochote na takribana watu zaidi ya milioni 300 huugua Malaria kila mwaka na milioni 1 hufariki hasa katika bara la Africa. Mbu wameua watu mashuhuri wa enzi hizo kama vile Alexander the Great miaka ya 323 BC, Oliver Cromwell, Vasco da Gama na David Livingstone na wengineo.

6: Kikawaida MBU husikia raha sana anapohisi harufu ya carbon dioxide sehemu fulani na huifata inapotokea akijua kuna uwezekano wa damu kupatikana kwa ajili ya kunyonya na kurutubisha mayai. Carbon dioxide hii hutolewa na viumbe wengi wenye damu nyekundu akiwemo mwanadamu.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: