Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Nkaya Bendera aliyekutwa na mauti jana katika hospitali ya taifa Muhimbili unatarajiwa kuzikwa Jumapili katika eneo la Manundu wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.


Akizungumza  nyumbani kwa marehemu Sinza jijini Dar es Salaam unapofanyika msiba, mdogo wa marehemu Allan Michael Bendera amesema taratibu za mazishi zinaendelea na mwili wa marehemu ambaye alikuwa akisumbuliwa na sukari utaagwa jumamosi katika hospitali Jeshi ya Lugalo na wadau mbalimbali saa nne asubuhi.

Wakizungumza  viongozi na watu wa karibu na marehemu wamesema kuwa kifo hicho ni pigo kwa taifa kumpoteza mtu mchapakazi na mwenye kujituma ambaye siku zote alikuwa nguzo ya maendeleo katika jamii.

Marehemu Joel Bendera ameacha mke na watoto watatu na atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa serikali na jamii kwa ujumla katika idara mbalimbali alizofanyia kazi pamoja na mchango wake mkubwa katika tasnia ya michezo.

Credit - ITV
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: